Swahili
Surah Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya count 36
وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ
( 1 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 1 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 1](style/islamic/icons/mp3.png)
Ole wao hao wapunjao!
الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ
( 2 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 2 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 2](style/islamic/icons/mp3.png)
Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.
وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ
( 3 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 3 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 3](style/islamic/icons/mp3.png)
Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.
أَلَا يَظُنُّ أُولَٰئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ
( 4 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 4 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 4](style/islamic/icons/mp3.png)
Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa
لِيَوْمٍ عَظِيمٍ
( 5 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 5 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 5](style/islamic/icons/mp3.png)
Katika Siku iliyo kuu,
يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ
( 6 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 6 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 6](style/islamic/icons/mp3.png)
Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?
كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ
( 7 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 7 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 7](style/islamic/icons/mp3.png)
Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.
وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ
( 8 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 8 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 8](style/islamic/icons/mp3.png)
Unajua nini Sijjin?
كِتَابٌ مَّرْقُومٌ
( 9 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 9 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 9](style/islamic/icons/mp3.png)
Kitabu kilicho andikwa.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
( 10 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 10 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 10](style/islamic/icons/mp3.png)
Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha!
الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ
( 11 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 11 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 11](style/islamic/icons/mp3.png)
Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.
وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ
( 12 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 12 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 12](style/islamic/icons/mp3.png)
Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.
إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ
( 13 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 13 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 13](style/islamic/icons/mp3.png)
Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale!
كَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ
( 14 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 14 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 14](style/islamic/icons/mp3.png)
Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma.
كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ
( 15 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 15 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 15](style/islamic/icons/mp3.png)
Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi.
ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ
( 16 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 16 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 16](style/islamic/icons/mp3.png)
Kisha wataingia Motoni!
ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ
( 17 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 17 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 17](style/islamic/icons/mp3.png)
Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha.
كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ
( 18 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 18 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 18](style/islamic/icons/mp3.png)
Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin.
وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ
( 19 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 19 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 19](style/islamic/icons/mp3.png)
Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin?
كِتَابٌ مَّرْقُومٌ
( 20 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 20 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 20](style/islamic/icons/mp3.png)
Kitabu kilicho andikwa.
يَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ
( 21 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 21 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 21](style/islamic/icons/mp3.png)
Wanakishuhudia walio karibishwa.
إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ
( 22 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 22 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 22](style/islamic/icons/mp3.png)
Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.
عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ
( 23 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 23 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 23](style/islamic/icons/mp3.png)
Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.
تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ
( 24 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 24 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 24](style/islamic/icons/mp3.png)
Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,
يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ
( 25 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 25 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 25](style/islamic/icons/mp3.png)
Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri,
خِتَامُهُ مِسْكٌ ۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ
( 26 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 26 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 26](style/islamic/icons/mp3.png)
Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana.
وَمِزَاجُهُ مِن تَسْنِيمٍ
( 27 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 27 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 27](style/islamic/icons/mp3.png)
Na mchanganyiko wake ni Tasniim,
عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ
( 28 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 28 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 28](style/islamic/icons/mp3.png)
Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa.
إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ
( 29 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 29 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 29](style/islamic/icons/mp3.png)
Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini.
وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ
( 30 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 30 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 30](style/islamic/icons/mp3.png)
Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana.
وَإِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمُ انقَلَبُوا فَكِهِينَ
( 31 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 31 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 31](style/islamic/icons/mp3.png)
Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.
وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَٰؤُلَاءِ لَضَالُّونَ
( 32 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 32 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 32](style/islamic/icons/mp3.png)
Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea.
وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ
( 33 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 33 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 33](style/islamic/icons/mp3.png)
Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.
فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ
( 34 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 34 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 34](style/islamic/icons/mp3.png)
Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri,
عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ
( 35 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 35 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 35](style/islamic/icons/mp3.png)
Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.
هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ
( 36 ) ![Swahili - Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 36 Al-Mutaffifin (Those Who Deal in Fraud) - Aya 36](style/islamic/icons/mp3.png)
Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda?